Zitto Kabwe.
KIONGOZI Mkuu wa Chama Cha
ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, katika
kile kilichoonekana kuwapa kijembe Chadema, akisema kutaka nchi kunyimwa
misaada ni uhayawani, kwani vita dhidi ya kuminywa kwa demokrasia
inapaswa kupiganwa ndani.
Zitto alitoa kauli hiyo kupitia akaunti
yake katika Mtandao wa Kijamii wa Twitter, ikiwa ni siku moja tu baada
ya Chadema kupitia kwa mwanasheria wake, Tundu Lissu kuitaka Jumuia ya
Kimataifa kuinyima Tanzania misaada kufuatia kitendo cha kukamatwa na
kufunguliwa mashtaka kwa viongozi wa upinzani, hasa kutoka chama chao.
“Huu ni uhayawani, hii ni nchi huru,
kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu ni upuuzi na umazwazwa,
tupambane ndani kuleta demokrasia,” aliandika Zitto.
Hata hivyo, kufuatia kauli hiyo baadhi
ya watumiaji wa mtandao huo walianza kumuuliza maswali kadha Zitto
ambaye aliwajibu na kuufanya mjadala huo kuwa mrefu, baadhi wakimuunga
mkono na wengine wakipingana naye.
0 comments:
Post a Comment