Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni (kushoto)
akiwauliza maswali abiria wa basi la Safari Express lifanyalo safari
zake Dar es Salaam – Arusha, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza
katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, Pwani.
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Masauni akiwa ameambatana na Kamanda wa
Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus
Musilimu, alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha
Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo, kwa
ajili ya kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo
mwaka jana.
Masauni (kushoto) akimuuliza maswali Dereva wa basi la Safari Express.
“Mwaka jana nilipofanya ziara kituoni
hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa
magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini
hakuna mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha
usalama wa abiria,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;
“RTO ameshindwa kuendana na kasi ya awamu
ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya
kinidhamu, hatutati uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania.”
Masauni (kulia) akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi, Jonathan Shana.
Masauni mara baada ya ukaguzi wa kituo
hicho, aliendelea na ziara yake mkoani Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa
aina hiyo mjini Chalinze na baadaye Msata na kuimalizia ziara yake
Bagamoyo.
Akiwa mjini Chalinze, Masauni
alizungumza na waendesha bodaboda na kuwapa maelekezo kuhakikisha
wanafuata sheria za usalama barabarani kwa kutobeba mishikaki, uvaaji wa
kofia ngumu na pia kufuata sharia zote za usalama barabarani.
Masauni (kulia) akizungumza na waendesha bodaboda wa Mji wa Chalinze, wakati wa ziara yake.
“Mmenihakikishia kwa wale ambao hamkua
na kofia ngumu kuwa mkitoka hapa mtakwenda kuzitafuta, hakikisheni
mnafanya hivyo kwa usalama wenu pamoja na abiria mnaowabeba, ipendeni
kazi yenu kwa kuheshimu sharia za usalama barabarani,” alisema Masauni.
Akiwa njiani kuelekea Chalinze mpaka
Bagamoyo, Masauni ambaye gari yake ilitolewa namba zinazomtambulisha
nafasi yake (NWMNN), na kuweka namba za kawaida ili kujua kama
akiendesha kwa mwendokasi barabarani matrafiki watalisimamisha gari
lake, hata hivyo askari wa usalama barabarani sehemu kubwa hawakuwepo
barabarani na pia waliokuwepo hawakuweza lisimamisha gari lake.
Masauni
(aliyevaa suti) akiwa katika ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi
cha Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani ambapo alifanya ziara ya kushtukiza
kituoni hapo.
Kutokana na hatua hiyo, Masauni
akagundua kuwa kuna uzembe mkubwa unaofanywa na matrafiki mkoani humo
kwa kutofanyakazi zao kwa umakini, na kwa uzembe huo ndio chanzo cha
ajali zinazotokea barabarani mara kwa mara.
Akizungumza na matrafiki wilayani
Bagamoyo ambao walifanya uzembe huo, aliwataka wabadilike haraka
iwezekanavyo kufuata wajibu wao, na pia alitoa siku tatu kuhakikisha
wanawakamata waendesha bodaboda wote ambao wanavunja sheria za usalama
barabarani, na pia baada ya operesheni hiyo apewe ripoti haraka
iwezekanavyo, na muda wowote atafanya ziara ya kushtukiza kuona kama
maelekezo hayo wameyafanyia kazi.
Masauni
akimpa maelekezo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) wakati alipokua
anazungumza na askari wa usalama barabarani katika eneo la Sanzale,
Bagamoyo.
“Bodaboda nimeziona nyingi zinapita
hapa zikiwa zinavunja sheria, madereva na abiria hawajavaa kofia ngumu,
na nyie mpo hapa mnaziangalia, sasa nawaagiza mtekeleze maagizo
niliyotoa na pia sio nyie tu bali nchi nzima wahakikishe wanayakagua
magari pamoja na bodaboda, na atakaepuuza atutacheka nae, tutapambana
nae,” alisema Masauni.
Kwa upande wake Kamanda Msilimu,
alisema ameyapokea maagizo yote na atahakikisha anayafanyia kazi
ipasavyo kwa kuwasimamia matrafiki wote nchini kwa umakini mkubwa
0 comments:
Post a Comment