Thursday 20 July 2017

VIGOGO SIMBA KURUDI RUMANDE


Kesi ya madai ya utakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa Simba, Rais wa Evans Aveva na Makamu Rais, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ imetajwa leo Julai 20 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.

Aveva peke yake aliweza kufika mahakamani hapo wakati wa kesi hiyo na taarifa za nje ya mahakama zimeeleza kwamba Kaburu akishindwa kufika mahakamani kutokana na kudaiwa kuwa ni mgonjwa.

Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande baada ya kesi yao kuahirishwa na sasa watarejeshwa mahakamani hapo Julai 31, mwaka huu.

Kabla ya kesi hiyo kutajwa wanachama wa Simba walianza kufika mahakamani mapema ili kujua hatima ya viongozi wao.

Awali kulikuwa na taarifa huenda leo wangepata ahueni na kuachiwa kwa dhamana.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive