“Tumechoka kuchezewa.” Hayo ni maneno ya Rais John Magufuli wakati akizindua rasmi maonyesho ya 41 ya kimataifa ya biashara huku akisisitiza maonyesho hayo yatumike kama chachu ya maendeleo.
“Tumechoka, tumechezewa mno, lakini tumechezewa kwa muda mrefu na tumechezewa kwa sababu tumeamua,” amesema.
Ameyasema hayo leo (Julai 1) wakati akihutubia katika viwanja vya Sabasaba.
Pamoja na kusisitiza utajiri ambao Tanzania inao, Rais amewataka wawekezaji walioshiriki maonyesho hayo kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ipo salama.
“Maonyesho haya yatumike kama chachu ya maendeleo,” amesema.
0 comments:
Post a Comment