Baada ya Serikali kukusudia kupeleka Bungeni muswada wa Sheria utakaofuta Sheria iliyoianzisha TLS mwaka 1954 ikiwa ni pamoja na kutengenisha shughuli za Uwakili na Chama hicho, Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema hatua hiyo inakusudia kubadilisha muelekeo wa taaluma ya Sheria na kuminya Uhuru wa Mawakili kuwatetea Wananchi.
Tundu Lissu alisema:>>>Baada
ya kuletewa na Wizara ya Katiba na Sheria kitu wanachokiita Bango
Kitita chenye mapendekezo ya kufanyia marekebisho makubwa katika
utaratibu mzima wa Taaluma ya Sheria katika Tanzania. Mapendekezo ambayo
tumeletewa ni makubwa kwa sababu yataleta mabadiliko makubwa sana
katika mfumo mzima wa Taaluma ya Sheria.
“Tumekuwa na Chama cha Mawakili
wa Tanganyika ambacho kinashughulikia masuala yote yanayohusu maslahi
ya Mawakili pamoja na masuala yanayohusu Utawala wa Sheria. Mawakili na
Chama chao kwa mfumo wa kisheria na Katiba wa kwetu ni sehemu kamili ya
mfumo wa utendaji Haki.
“Ili Mawakili waweze kusaidia watu kupata Haki zao
wasiingiliwe katika masuala yao ya kitaaluma. Waweze kusaidia jamii
kupata Haki bila ya wao kuwa na hofu kwamba mambo yao, maslahi yao, Haki
zao zitaathiriwa. Ndiyo maana ya kuwa na Chama huru cha Mawakili na
kuwa na utaratibu Huru wa kisheria unaohakikisha kwamba Serikali
haiingilii mambo ya Mawakili.” – Tundu Lissu.
0 comments:
Post a Comment