Rais Magufuli leo July 1, 2017
amefungua rasmi maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara ambayo hufanyika
kila mwaka katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Kilwa Road DSM na
kupata nafasi ya kuhutubia na kuyapongeza makampuni yanayoshiriki
maonesho hayo.
Katika hotuba yake kwenye maonesho hayo Rais JPM amewaomba
waandaaji na viongozi kuweka mipango ili kujenga Hotel na Majengo mapya
katika viwanja hivyo akiwataka wajenge kiwanda kitakachowasaidia
watanzania kupata ajira na kukarabati majengo kama yamechakaa.
“Haingii akili
wao ndio wanatusisitizia mambo ya biashara na viwanda na theme ya mwaka
huu inazungumzia kukuza biashara na maendeleo ya viwanda sasa wao badala
ya kuzungumza juu ya maendeleo ya viwanda wanataka wajenge Hotel hapa,
watengeneze majengo mapya sasa. Sijaelewa.
“Sasa kama hizo hela zipo basi mzipeleke mkajenge kiwanda
cha mfano. Haya majengo yaliyopo ambayo mnayaona yamechakaa hawa
wanaokuja kuonesha bidhaa zao wapeni bure wajenge ili kila mwaka wawe
wanaonesha.
“Hiyo Hotel kwani mkijenga
lazima walale hapa hapa? Mnaweza kujenga Hotel hapa bado wakaenda
Hotelini mjini. Mimi nilifikiri ili kujenga jenga majengo fikirieni
zaidi katika kujenga viwanda kwa ajili ya mfano wa kuonesha Wizara kweli
iko mbele kwa kujenga viwanda.
“Haya majumba yanaweza yakawa siyo mazuri sana lakini ni
mazuri kwa watu wa Tanzania ambao wanataka kuona bidhaa. Yanayowaleta
hapa siyo majumba Watanzania wanakuja hapa kuangalia Tecknolojia na
vifaa vilivyomo.
“Inawezekana mimi nipo
tofauti mnisamahee lakini katika muelekeo wangu ninaona hizo hela
mnataka kuzitumia vibaya. Mwenyekiti nimekuteuwa juzi umeshaanza
kufikiria majengo hapa pamoja na Body yako mnanifanya nifikirie zaidi.
“Nimeshasema, nimewapongeza na ninawapongeza washiriki
wote basi tuangalie masuala ambayo ni very positive kwa Taifa hili
tunataka kuwa na viwanda vingi na siyo Hoteli nyingi.” – Rais JPM.
0 comments:
Post a Comment