WATU na vipaji vyao bwana! Huku akiwa amefikisha miezi saba tangu alipoingia katika ikulu ya Marekani ‘White House’ hatimaye mchoro wa kwanza kabisa kuchorwa unayomuonyesha Rais Donald Trump akiwa oval ‘ofisi ya rais’ na mchoro wa mke wake, Melania upo njiani kuelekea ikulu.
Michoro hiyo miwili ni zawadi ya kipekee iliyotolewa na bunge linaloongozwa na Bwana Mike Kelly huku michoro hiyo iliyochorwa kwa ustadi mkubwa ikiwa imechorwa na jamaa anayeitwa Barry Wingard.
Mara baaada ya kukamilisha michoro hiyo, Wingard alikwenda ofisini kwa Kelly huko 1600 Pennsylvania Ave
ambapo alimkabishi michoro hiyo aliyoichora kwa kutumia rangi za
mafuta. Michoro hiyo ilichukuliwa na kuanza kupelekwa ikulu ambapo Trump mwenyewe ataamua kama itatundikwa humo au la.
0 comments:
Post a Comment