Paris Saint-Germain wanataka
kuwapiku Manchester City katika dakika za mwisho na kumsajili Dani
Alves. Beki huyo kutoka Brazil alionekana kukaribia kuhamia City lakini
PSG huenda wakamchukua (Le10Sport).
Wakala wa James Rodriguez
amewaambia Liverpool, Manchester United, Inter Milan, Juventus,
Manchester City na PSG kuwa wanaweza kumsajili kiungo huyo wa Real
Madrid, lakini hakuna kati ya timu hizo iko tayari kutoa euro milioni 75
wanazotaka Real, ambao wanataka kumuuza kutokana na kuwasili kwa Dani
Caballos (SPORT).
Beki wa Southampton Virgil van Dijk ameiambia klabu yake kuwa anataka kuhamia Liverpool tu (Mirror).
Manchester
United wapo tayari kuwapiga kumbo jingine Chelsea kwa kumsajili James
Rodriguez. Chelsea na PSG zinamtaka mchezaji huyo lakini James mwenyewe
angependa kwenda kwa Mourinho (Express).
Baada ya kuwazidi kete
Chelsea katika kumsajili Romelu Lukaku, Manchester United wamemsajili
Lomelu Lukakuwanataka kuwapiku tena katika kumsajili kiungo Tiemoue
Bakayoko kutoka Monaco, ambao wamekasirishwa na kasi ndogo ya Chelsea
kumfuatilia mchezaji huyo. United watamchukua ikiwa watashindwa kumpata
Nemanja Matic kutoka Chelsea (The Sun).
James Rodrigues anataka kuhakikisha anaondoka Real Madrid katika saa
48 zijazo ili asisafiri na Real Madrid kwenda Marekani katika mechi za
kabla ya kuanza kwa msimu (AS).
Arsenal wamekubaliana maslahi
binafsi na Thomas Lemar ya mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki, lakini
bado hawajafikia makubaliano na Monaco (the Sun).
Celta Vigo wanafikiria kumchukua winga wa Borussia Dortmund Emre Mor ambaye pia amehusishwa na Liverpool (Atlantico).
Dani
Ceballos, 20, amekubali mkataba wa miaka sita kujiunga na Real Madrid
kutoka Real Betis na atakamilisha mkataba wa euro milioni 18. Barcelona
walikuwa 'wakimchombeza' mchezaji huyo (Marca).
Antonio Rudiger
anakaribia kukamilisha uhamisho wake kutoka Roma kwenda Chelsea kwa
pauni milioni 34 na mkataba utakamilika katika saa 24-48 zijazo (Sky).
Arsenal
wameweka wazi kuwa hawatomuuza Alexis Sanchez au Alex Oxlade-
Chamberlain kwenda katika timu yoyote hasimu ya EPL. Sanchez ananyatiwa
na Manchester City huku Oxlade-Chamberlain akihusishwa na Liverpool
(Daily Star).
Arsenal watakuwa tayari kumuuza Alexis Sanchez kwenda Manchester City ikiwa tu watatoa pauni milioni 80 (Mirror).
Arsenal
wameongeza dau lao hadi pauni milioni 40 kutaka kumsajili winga Thomas
Lemar, 21 kutoka Monaco, baada ya pauni milioni 35 za awali kukataliwa
(L'Equipe).
Meneja Antonio Conte atarejea Chelsea siku ya Jumatatu
kutoka likizo na kutaka mazungumzo na klabu hiyo kuhusu kushindwa
kumsajili Romelu Lukaku kutoka Everton (Express).
Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, 31, amefanya vipimo vya afya Everton (Sky Sports).
Zlatan Ibrahimovic, 35, huenda akapewa mkataba mpya na Manchester United baada ya kupona jeraha la goti (Mirror).
Tottenham
wamesema kiungo wao Eric Dier, 23, hauzwi kwa bei yoyote. Hii ni baada
ya kuhusishwa na Manchester United kwa pauni milioni 50 (Mail).
Jose
Mourinho ameongeza juhudi za majadiliano kutaka kumsajili James
Rodriguez, 25, kutoka Real Madrid. Real wanataka pauni milioni 62
(Independent).
Newcastle wamekuwa na mazungumzo na Middlesbrough ya kutaka kumsajili
winga Adama Traore, 21 ambaye huenda akagharimu hadi pauni milioni 20
(Chronicle).
Newcastle wapo tayari kulipa euro milioni 20 kumsajili Andreas Samaris kutoka Benfica (O Jogo).
Kiungo
wa Bayern Munich Douglas Costa anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa
mkopo kwenda Juventus na huenda akahamia moja kwa moja baadaye kwa euro
milioni 40 (La Stampa).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara
zitakapothibitishwa.
0 comments:
Post a Comment