Mshambuliaji wa Manchester United na
mshikilizi wa rekodi ya mabao Wayne Rooney amejiunga na Everton, miaka
13 tangu ahame klabu hiyo.
Rooney mwenye umri wa miaka 31 alichezea Manchester United mara 559 akifunga mabao 253.
Alishinda ligi tano za Primia tangu aihame Everton kwa pauni milioni 27 mwaka 2004.
"Ninahisi vizuri kurudi, sitangoja kukutana na wenzangu, kuingia mazoezini na kisha kuingia uwanjani kucheza." alisema Rooney.
Rooney anarejea Everton waaati Man U ina mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku kwa pauni milioni 75.
Anakuja tz uyooooooo
ReplyDelete