Romelu Lukaku anatarijiwa kufanyiwa
ukaguzi wa kimatibabu na Manchester United baada ya kukubali kuilipa
Everton kitita cha pauni milioni 75 ili kumsajili mshambuliaji huyo wa
Ubelgiji.
Makubaliano hayo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
24, yalioripotiwa awali na BBCsport siku ya Alhamisi yanaaminika
kushirikisha marupuru mengine ya pauni milioni 15.
United imesema
kuwa wamefurahishwa na makubaliano hayo na kwamba usajili wake utafanywa
tu baada ya kufanyiwa ukaguzi wa matibabu na makubaliano ya kibinafsi.
Chelsea
ilikuwa imefikisha kiwango kilichokuwa kikitolewa na Manchester United
lakini wakaonekana kushindwa kumsajili mchezaji wao wa zamani.
The
Blues hawakuwa tayari kufikisha kiwango kilichotakiwa na ajenti wa
mchezaji huyo Mino Riaola iwapo mchezaji huyo angeelekea Old Trafford.
Tangazo jingine litafanywa katika muda wowote, iliongezea United.
Mkufunzi
wa Manchester United Jose Mourinho alikuwa mkufunzi wa Chelsea wakati
timu hiyo ilipomuuza mchezaji huyo kwa Everton kwa pauni miloni 28
mnamo mwezi Julai 2014.
Mbelgiji huyo alifunga mabao 25 katika
ligi ya Uingereza msimu uliopita na Manchester United wamekuwa wakitaka
kumsajili msimu wote uliopita.
United wanaharakisha usajili wa mchezaji huyo kabla ya kuondoka kuelekea Marekani kwa maandilizi ya msimu ujao siku ya Jumapili.
Wayne
Rooney hatarajiwi kuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha United kwa
ziara hiyo kwa kuwa anatarajiwa kurudi Everton kwa uhamisho wa bure.
Karibu Trafford lukaku
ReplyDelete