Saturday, 8 July 2017

OMOG KUTUA LEO KWA MAANDALIZI YA LIGI KUU VPL


Image result for omog simba

UONGOZI wa klabu ya Simba umesema kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog anatarajiwa kuwasili nchini leo kuanza kazi ya kukiandaa kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.



Wachezaji wa timu hiyo walianza mazoezi juzi bila kuwapo kwa kocha huyo ambaye alienda Cameroon kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa ligi msimu uliopita.

Kaimu Makamu wa rais wa klabu hiyo, Iddy Kajuna, alisema jana kuwa wanategemea kocha huyo ataingia leo usiku.

"Huwenda Jamatatu akaanza programu yake kutegemea na vile alivyoandaa..., tunategemea kesho usiku (leo) atawasiri kwa sababu tumewasiliana naye," alisema Kajuna.

Simba imepanga kuendelea kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini mpaka hapo mipango yao ya kwenda kuweka kambi ya muda nje ya nchi itakapokamilika.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive