Saturday 8 July 2017

TRUMP NA PUTIN MEZANI KUJADILI UCHAGUZI WA MAREKANI

Trump na Putin
Rais Trump wa Marekani na Putin wa Urusi wamejadiliana kwa mapana madai ya uingiliaji wa Urusi katika Uchaguzi wa Urais uliofanywa nchini Marekani mwaka uliopita.
Walifanya mashauriano hayo ana kwa ana pembezoni mwa mkutano wa viongozi wa mataifa 20 tajiri ulimwenguni ya G20 katika mji wa Hamburg.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, alitaja mashauriano hayo kama ya uwazi lakini akaeleza kuwa kwa sasa haijulikani iwapo mataifa hayo mawili yataelewana juu ya hasa kilichotokea.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, alisema Bwana Trump alikubali hakikisho la Bwana Putin kuwa Urusi haikushiriki katika kuhakikisha kuwa yeye, Trump, anachaguliwa kuwa Rais wa Marekani.
Mhariri wa BBC wa Marekani Kaskazini anasema kuwa anachoeleza Bwana Lavrov ni ukweli, ina maana kuwa Bwana Trump anakubali maelezo ya Urusi, kuliko amavyowaamini maafisi wake wa ujasusi.
Bwana Tillerson alisema kuwa viongozi hao wawili walichangamana kwa haraka sana na kuwa walielewana bila wasiwasi wo wote.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive