Halima Mdee
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Kisutu leo asubuhi ili kusomewa mashtaka ya kesi yake inayomkabili.
Mdee, alikamatwa na Polisi siku sita
zilizopita kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi kwa madai
ya kumkashifu Rais John Magufuli.
Hapi aliagiza Mdee akamatwe na kuwekwa ndani kwa saa 48 kwa makosa hayo pamoja na ya uchochezi.
UPDATES
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea shtaka la kutoa lugha ya matusi Mbunge Halima Mdee, ambaye amekana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana ya Tsh. Milioni 10.
Akisoma shtaka hilo, Wakili wa
Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa alisema
mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo
Baada ya kukana shtaka hilo Hakimu
alisema mshtakiwa huyo ambaye wakili wake ni Peter Kibatala ana haki ya
kupewa dhamana, ndipo akadhaminiwa na madiwani wawili wa Chadema (majina
hayajapatikana) pamoja na yeye mwenyewe kwa bondi ya Tsh. Milioni 10
huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Julai 7 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment