
Mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa na Rais. John Magufuli
kujadiliana na
uongozi wa Barrick Gold Corporation akiwa na ujumbe wa
kampuni hiyo kabla ya
kuanza mazungumzo hayo leo jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
Majadiliano kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli
na wawakilishi kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation kuhusu madini
yanayochimbwa na kampuni hiyo nchini yameanza leo, Julai 31 jijini Dar
es Salaam.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa,
imesema kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria,
Profesa Palamagamba Kabudi na kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa
Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams.

Profesa Kabudi amekaririwa katika taarifa hiyo akisema wamejipanga
vizuri kujadiliana na Barrick juu ya madai ya Tanzania katika biashara
ya madini ya kampuni hiyo nchini na itahakikisha inasimamia masilahi ya
nchi ipasavyo.
kwa mazungumzo hayo leo.
Imeelezwa Williams ameshukuru uwepo wa majadiliano hayo akisema
Barrick imepokea madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na ipo tayari
kujadiliana na kufikia makubaliano yenye masilahi kwa pande zote mbili.
Prof. Kabudi akizungumza akiwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni hiyo, Richard Williams, kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo leo.
Rais aliunda kamati hiyo baada ya kupokea ripoti za kamati zingine
mbili, moja ilichunguza mchanga wa madini (makinikia) na nyingine ya
kitaalamu iliyochunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu mchanga
huo unaosafirishwa nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment