Mambo ya umiliki wa Klabu ya Simba pamoja na kubadili mfumo wa
uendeshaji wa klabu hiyo bado yanaendelea kupata kipingamizi ambapo
wazee wa klabu hiyo wameliamsha dude kwa mara nyingine.
Baraza la Wazee wa Simba, leo Jumapili wamekutana na waandishi wa
habari na kusema msimamo wao ni kuwa hawatambui mikutano iliyotajwa kuwa
itafanyika Agosti 13 na 10, mwaka huu kwa kuwa umeagizwa kufanyika na
viongozi wanaokaimu nafasi ya uongozi wa juu klabuni hapo huku viongozi
wenyewe wakiwa bado mahabusu.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika makao
makuu ya Klabu ya
Simba, Mzee Hamis Kilomoni
alisema hawawezi kukubali na wala hawatambui
hiyo mikutano ya wanachama iliyopangwa kufanyika
siku hizo mbili.
“Viongozi wetu wakuu wapo mahabusu, tutafanyaje mkutano wakati tukiwa
hatujui hatima ya viongozi wa juu, haiwezekani, pia kuhusu umiliki wa
klabu, tulishampa Mo (Mohamed Dewji) nafasi atuletee hoja zake mezani
juu ya nia yake ya kutaka kuimiliki Simba lakini hajafanya hilo, hivyo
sisi hatutakubali na wala hatuafiki mkakati huo, alisema mzee Kilomoni.
0 comments:
Post a Comment