KOCHA Mkuu wa Yanga, George Lwandamina anatarajia kuanza program ya uwanjani, maalumu kwa wachezaji wake wapya kushika mfumo na mbinu anazozitumia za uchezaji.
Timu hiyo imefanya usajili mdogo kwa kuziboresha baadhi za nafasi
ikiwemo ya ushambuliaji ambayo imemsajili, Ibrahim Ajibu kwa mkataba wa
miaka miwili akitokea Simba akiwa mchezaji uhuru.
Yanga itaanza mazoezi hayo ya uwanjani asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
baada ya kumaliza program ya gym waliyoifanya kwa wiki mbili, ambapo
wachezaji hao wapya akiwemo Ajibu watapata nafasi ya kujua mbinu
mbalimbali za Lwandamina tofauti na zile walizokuwa wakizitumia walipokuwa kabla ya kutua Yanga.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema timu hiyo itaanza mazoezi ya uwanjani baada ya wachezaji kutengeneza fiziki ya kutosha gym.
Saleh alisema, program ya mazoezi ya uwanjani muhimu kwa wachezaji
ambao bado hawajaijua falsafa (philosophy) ya kocha ambayo anaitumia,
hivyo ni vema wakaanza mapema washike na wazoee.
“Kila mchezaji akitoka kwenye timu moja na kwenda kwingine ni lazima
apate ugumu wa kuzoea ‘philosophy’ ya kocha mpya atakayekutana naye.
“Kama unavyojua kila kocha ana mfumo na aina ya uchezaji ya soka la
pasi la haraka au taratibu, hivyo basi kocha amepanga kuanza nao kesho
(leo) kwa kuwapa mazoezi ya uwanjani.
“Ninaamini kabisa kwa wiki hizi mbili ambazo timu ilikuwa gym
ikifanya mazoezi ya gym kwa ajili ya kuongeza fiziki, wachezaji watakuwa
fiti tayari na kuanza program ya mazoezi ya uwanjani kucheza mpira ili
miili yao ifunguke,” alisema Saleh.
Mtengeneze baba amuuwe yule anayejiita ati Simba.
ReplyDelete