Baada ya tetesi ndani ya wiki kadhaa, hatimaye Klabu ya Yanga imesajili kipa chipukizi, Ramadhani Kabwili.
Kipa huyo aliyekuwa akiidakia timu ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys amesaini
mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu hiyo yenye makao makuu mitaa ya
Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kabwili anaungana na kipa mwingine
mpya, Mcameroon Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon na
Benno Kakolanya ambaye huu utakuwa msimu wa pili tangu asajiliwe
akitokea Tanzania Prisons ya Mbeya.
Kabwili na Rostand wote wanasajiliwa
kuchukua nafasi za makipa wa muda mrefu wa Yanga, Ally Mustafa ‘Barthez’
na Deogratius Munishi ‘Dida’ waliomaliza mikataba yao na kuruhusiwa
kuondoka.
Ohhh! Huyu Dogo yupo good.
ReplyDelete