NAHODHA na mchezaji wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, rasmi ni kocha msaidizi wa timu hiyo.
Nsajigwa aliyekuwa anaifundisha timu ya vijana ya U20 anakuwa kocha wa timu hiyo akichukua nafasi ya Juma Mwambusi aliyekuwa anakinoa kikosi hicho.
Yanga inaachana na Mwambusi baada ya
mkataba wa kuendelea kuifundisha timu hiyo kumalizika mwishoni mwa msimu
uliopita wa Ligi Kuu Bara.
Moja kati ya vyombo vya habari hapa nchini, kilimshuhudia Nsajigwa jana akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Nsajigwa alionekana akitoa baadhi ya
maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo akisaidiana na kocha wa viungo wa
timu hiyo, Mzambia, Noel Mwandila.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti
hili limezipata, kabla ya mazoezi hayo kuanza Nsajigwa alitambulishwa
kwa wachezaji wa timu hiyo.
“Nsajigwa rasmi ni kocha msaidizi wa
Yanga atakayekuwa anasaidiana na Lwandamina, Mwandila na Mwambusi
hatakuwepo na timu hiyo tena,” alisema mtoa taarifa huyo.
chombo hicho mara baada ya mazoezi hayo
kumalizika, kilimtafuta Nsajigwa kuthibitisha hilo, akasema: “Mimi sina
taarifa rasmi juu ya hilo suala la kuwa kocha msaidizi, tusubirie kwanza
kama ikiwa hivyo basi nitatoa taarifa rasmi.”
0 comments:
Post a Comment