Wednesday, 12 July 2017

HUU NDIYO UKWELI WA FLOYD MAYWEATHER


Jina lake halisi anaitwa Floyd Joy Sinclair lakini wengi wanamfahamu kwa jina la Floyd Mayweather, alizaliwa Februari 24, 1977 huko Grand Rapid, Michigan nchini Marekani kutoka kwa mama, Deborah Sinclair na baba Floyd Mayweather Sir.
Ana urefu wa futi 5 na nchi 8 na uzito wa kilo 68.5, akiwa ni bondia mwenye rekodi ya aina yake katika masumbwi ya uzito wa Middle Weight na Super Feather Weight.
Mpaka sasa ameshashiriki mapambano 49, hajapoteza pambano hata moja, na kati ya hayo, 26 ameshinda kwa ‘knock out’, huku akitwaa mikanda 15 ya ngazi ya dunia, mitano kati ya hiyo akiishikilia kwa miaka minne mfululizo.
Mayweather ameingia katika rekodi ya mabondia wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi kwa mwaka, pambano lake la mwisho la mwaka 2015, kabla ya kustaafu, alimpiga bondia kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao mwenye urefu wa futi tano na nchi 5, na uzito kilo 66, baada ya kuibuka mshindi katika pambano hilo mashabiki walimpachika jina la The Best Ever au T.B.E.
Bondia huyu ambaye pia ni mjasiriamali ana miliki akaunti moja ya benki yenye zaidi ya dola milioni 123 ndani yake.
Mayweather ni kiongozi wa kundi liitwalo The Money Team (T.M.T), na upande wa pili wa maisha ya kimapenzi,  bado hajaoa hadi sasa ila ni baba wa watoto wanne kwa wanawake tofauti, mpenzi wake wa awali Jossie Harris amezaa naye watoto wawili wa kiume Koraun na Zion, na mmoja wa kike anayeitwa Jirah.
Mtoto wake wa mwisho anaitwa Iyyana, amezaa na mpenzi wake mwingine, Mellisia Brim. Alishawahi kutumikia kifungo jela huko Las Vegas kwa kosa la unyanyasaji na vurugu.
Share:

1 comment:

Ads

Blog Archive