STAA wa zamani wa Manchester
United, Wayne Rooney ambaye ametua nchini leo Jumatano na kikosi cha
timu yake mpya ya Everton tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor
Mahia kesho Alhamisi.
Wakati Rooney akitua nchini, Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), limemteua mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania
mwenye beji ya Fifa, Israel Mujuni Nkongo, kuchezesha mechi hiyo ya
Everton na Gor Mahia.
Rooney na wachezaji wengine wa Everton
pamoja na benchi la ufundi, wametua nchini leo Jumatano kwa ajili ya
kuwapa burudani Watanzania kesho Alhamisi.
Mechi hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya
Michezo ya Kubashiri ya SportPesa, inatarajiwa kupigwa kesho Alhamisi
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas,
amesema mbali na Nkongo kuwa mwamuzi wa kati, wasaidizi wake watakuwa ni
Ferdinand Chacha na Frank Komba. Elly Sasii atakuwa mwamuzi wa akiba,
huku Michael Wambura akiwa kamishna wa mchezo huo.
Kuelekea mchezo huo, Mkurugenzi wa
Utawala na Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba, amesema:
“Maandalizi yanakwenda vizuri, Gor Mahia wamekuja leo (jana Jumanne)
mchana, wakati kesho (leo Jumatano) asubuhi, tunatarajia kuwapokea
Everton.”
Katika mchezo huo ambao viingilio
vitakuwa ni Sh 3,000 na 8,000, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa
Rais wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu.
0 comments:
Post a Comment