Monday 24 July 2017

HUENDA CHELSEA ISIKANYAGE TENA CHINA


Mamlaka za masuala ya mwasiliano nchini China inasemekana zimeamuru mitandao ya nchini humo kufuta habari zote zinazohusiana na klabu ya Chelsea.
Hii inakuja baada ya kiungo Mbrazil wa Chelsea Kennedy kupost video ambazo ziliwadhihaki Wachina na kutafsiriwa kama ubaguzi au matusi kwa raia wa nchi hiyo.
Pamoja na klabu ya Chelsea kuomba msamaha kutokana na tukio hilo lakini inasemekana nchini China bado Chelsea wanajadiliwa na wizara husika na adhabu kubwa huenda ikawakumba.
Nchini China wanachukulia serious sana masuala ya makosa ya kimtandao na mara zote wamekuwa wakitoa adhabu kali kwa watu wanaofanya makosa ya kimtandao.
Kennedy amewaomba msamaha Wachina lakini pia klabu ya Chelsea iliandika ujumbe kuomba msamaha kwa taifa hilo lakini hadi sasa Wachina wamekaa kimya hawajawajibu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive