Manchester United imeshinda kwa penalti 2-1 dhidi ya
Real Madrid katika mechi za michuano ya ICC iliyopigwa jijini
California, Marekani.
Ndani ya dakika 90 timu hizo zilimaliza kwa sare ya 1-1
baada ya Jesse Lingard kutangulia kufunga na baadaye Casemilo
akaisawazishia Madrid.
Mechi hiyo iliyokuwa na mvuto wa aina yake De Gea alishuhudiwa akiokoa mikwaju ya penati na kuipa ushindi klabu yake ya Man U.
Anthony Martial alitumia juhudi binafsi na kumtengenezea pande Jesse Lingard na kuandika goli la kwanza.
Casemiro aliisawazishia Madrid kwa njia ya penalti baada ya mlinzi
mpya wa United Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la
hatari. Penalti saba kati ya kumi hazikuingia nyavuni.
REAL MADRID (4-3-3): Navas; Carvajal (Hakimi 46), Varane (Quezada
46), Nacho (Manu 46), Marcelo; Modric (Kovacic 46), Kroos, Isco (Oscar
46); Vazquez (Hernandez 46), Benzema (Gomez 46), Bale (Franchu 46).
Subs: Tejero, Gomez, Casilla, Mayoral, Zidane, Yanez.
MAN UTD (4-1-4-1): Romero (De Gea 46); Fosu-Mensah (Blind 46),
Bailly (Smalling 46), Jones (Lindelof 46), Darmian (Valencia 77);
Carrick; (Pogba 46) Lingard (Mkhitaryan 46), Fellaini, A Pereira
(Herrera 46, McTominay 52), Martial; Rashford (Lukaku 46). Subs:
Tuanzebe, J Pereira, Valencia, Mitchell.
Mabao ndani ya dakika 90: Lingard (dakika ya 45) na Casemiro (dakika ya 69) kwa penalty.
0 comments:
Post a Comment