Mshambuliaji wa Barcelona Neymar,
25, amewaambia wachezaji wenzake, Lionel Messi na Luis Suarez, kuwa
atabakia Barca baada ya wawili hao kumshawishi kutojiunga na Paris
Saint-Germain kwa uhamisho utakaovunja rekodi ya dunia wa pauni milioni
200. (Sport)
Cristiano Ronaldo amemtaka Neymar kutohamia PSG na kusubiri kwenda Manchester United wakati utakapowadia. (Diario Gol)
Meneja
wa Inter Milan Luciano Spalletti ameionya Manchester United kwa kusema
watoe pauni milioni 48 kama wanamtaka Ivan Perisic, vinginevyo wasahau
kumsajili winga huyo. (The Sun)
Arsene Wenger amedai kuwa PSG wanataka kumsajili Neymar kwa sababu wameshindwa kumsajili Alexis Sanchez. (Daily Mirror)
Monaco wamesema wanataka pauni milioni 55 kumuuza winga Thomas Lemar, 21, ambaye anasakwa na Arsenal. (Daily Star)
Manchester United wapo tayari kuwapa PSG pauni milioni 70 ili kumsajili kiungo Marco Verratti. (Daily Express)
Marco Verratti amesema chaguo lake la kwanza ni kwenda Barcelona, ingawa pia yuko tayari kwenda Manchester United. (Express)
Manchester United wapo tayari kupanda dau kumtaka kipa chipukizi wa Bolton Wanderers Jake Turner, 18. (The Sun)
Juventus
wameacha kumfuatilia kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic, 28 na hivyo
kutoa mwanya kwa Manchester United kukamilisha uhamisho wake. Chelsea
wamesema wanataka pauni milioni 40 ambazo Juve hawapo tayari kutoa.
(Telegraph)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ametoa "hakikisho la 100%"
kwa mashabiki kuwa kipa David de Gea atakuwepo Old Trafford msimu huu
mpya. (Telegraph)
Manchester United na Arsenal huenda wakapambana katika kumsajili winga wa Real Madrid Marco Asensio, 21. (Don Balon)
Deportivo
la Coruna wamempa mkataba wa miaka kumi Lucas Perez katika jitihada za
kumshawishi mshambuliaji huyo wa Arsenal kurejea katika klabu yake hiyo
ya zamani. (DXT Campeon)
Mazungumzo ya uhamisho wa mshambuliaji wa
Arsenal Alexis Sanchez, 28 kwenda PSG yameporomoka kutokana na bei
kubwa ya ada ya uhamisho na mshahara anaodai. (Le Parisien)
Arsenal wanajiandaa kupanda dau la takriban euro milioni 30 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho. (Record)
Chelsea
wataongeza bidii katika kutaka kumsajili kiungo wa Arsenal Alex
Oxlade-Chamberlain, 23, wiki hii ingawa huenda wakakabiliwa na ushindani
kutoka Manchester City. (Express)
Chelsea wanataka kuwazidi kete
Manchester United na AC Milan katika kumsajili mshambuliaji wa Fluminese
Ricjardlison. (Gianluca Di Marzio)
Jurgen Klopp amesema kiungo wake Emre Can haendi popote. (Liverpool Echo)
Liverpool wanasubiri kuona kama Southampton watakuwa tayari kuzungumzia uhamisho wa Virgil van Dujk. (Liverpool Echo)
West Brom wanajiandaa kutoa pauni milioni 10 kumsajili beki wa Manchester United Chris Smalling, 27. (Daily Star)
Matumaini
ya Liverpool kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita yamefifia baada
ya klabu hiyo kusisitiza kuwa haumuuzi mchezaji huyo. (Sky Sports)
fununu nyingine tukutane kesho tukijaaliwa. Asante
0 comments:
Post a Comment