Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya haki na maridhiano nchini Kenya TJRC Bethuel Kiplagat amefariki.
Kulingana na gazeti la daily Nation nchini Kenya ,bwana Kiplagat amefariki akiwa na umri wa miaka 82 katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Balozi Kiplagat ambaye aliwahi kuwa mwanadiplomasia na afisa wa serikali ya Kenya, alihudumu kama mwenyekiti wa TJRC kutoka 2009 hadi Novemba 2010.
Alijiuzulu baada kuchunguzwa kwa jukumu lake kuhusu unyanyasaji wa haki za kibinaadamu , hususan jukumu lake katika mauaji ya Wagalla 1984.
Kulingana na gazeti hilo alirudishwa kuiongoza tume hiyo hiyo licha ya pingamizi kutoka kwa wanachama wenzake wa tume hiyo 2012.
Alihudumu kama mjumbe maalum wa Kenya katika mpango wa amani nchini Somalia kati ya 2003 na 2005 na kuongoza bodi ya hazina ya utafiti wa matibabu barani Afrika kutoka 1991 hadi 2003.
Awali alikuwa amehudumu katika serikali ya rais Moi kwa takriban miaka 13 kutoka 1978-1991 kama balozi wa Kenya nchini Ufaransa , kamishna mkuu wa Uingereza na katibu wa kudumu katika wizara ya maswala ya nchi za kigeni.
Bwana Kiplagat alihusishwa na mauaji ambapo mamia ya raia wa Wajir waliuawa , huku wengine wakiteswa wakati wa operesheni ya usalama.
Alikuwa akihudumu kama katibu wa kudumu katika wizara ya mambo ya nje katika utawala wa rais Daniel Moi wakati huo.
Mnamo mwezi Agosti 2016, Kiplagat alimuandikia mkurugenzi wa mashtaka kufanya uchunguzi wa kina baada ya kutajwa katika ripoti ya TJRC
0 comments:
Post a Comment