
Baada ya headlines za muda mrefu kuhusiana na hatma ya kiungo
wa kimataifa wa Rwanda anayeichezea Dar es Salaam Young Africans Haruna
Niyonzima kuhusishwa kuhama Yanga na kujiunga na Simba baada ya mkataba
wake kumalizika.
Leo June 21 2017 Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa
ametangaza na kuweka wazi kuwa Haruna Niyonzima ambaye mkataba wake na
Yanga unamalizika July, wameshindwa kufikia makubaliano ya kumuongezea
mkataba mpya.
Hivyo ni rasmi sasa baada ya Haruna Niyonzima kuitumikia Yanga kwa
misimu sita mfululizo, atakuwa nje ya Yanga kuanzia msimu ujao wa
2017/18, bado haijajulikana rasmi Niyonzima atajiunga na timu gani
lakini kwa tetesi zinazoenea ni kuwa Niyonzima atajiunga na Simba.
0 comments:
Post a Comment