Wednesday 21 June 2017

SHEREHE YA KULA NYAMA ZA MBWA YAIBUA UTATA CHINA

wafanyabiashara ya nyama za mbwa wakiendelea na maandalizi.   
Sherehe ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin nchini China imeanza licha ya ripoti za awali ilionesha kuwa ilikuwa imepigwa marufuku mwaka huu.
Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi.
Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa.
Lakini wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo waliambia shirika la BBC hawajasikia lolote kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa.
Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote.
 
Wateja wa nyama ya mbwa wakibugia vipande vya nyama ya mbwa katika sherehe ya Yullin ya mwaka uliopita.
Siku ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo.
Mwanaharakati mmoja aliambia shirika la BBC kwamba alikatazwa na maafisa wa polisi kuingia katika soko la Dashichang ambapo inaaminika mbwa walikuwa wanauzwa.
Katika sherehe za miaka ya nyuma kumekuwa na mzozo kati ya wauzaji nyama ya mbwa na wanaharakati waliojaribu kuwaokoa mbwa waliopangiwa kuchinjwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive