Na Denis Massawe
Rais wa Marekani Donald Trump
amerejea kwenye Ikulu ya nchi hiyo siku ya Jumapili mchana baada ya kutoka mapumnzikoni
alikosheherekea siku ya baba duniani.
Trump alitumia siku ya baba
duniani kwenda Camp David tofauti na ilivyozoeleka kwa marais waliopita kwani
wengi wao walikuwa wakipumzika maeneo ya Maryland ambako ni mahususi kwa ajili
yao.
Katika safari hiyo rais Trump
aliambatana na mkewe Melania pamoja na mwanae Barron ambapo Melania alivaa blauzi
nyeupe mchanganyiko na Mizeituni, Maria
Jeans na viatu aina ya Manolo Blahnik.
Nae Barron alivaa kawaida tu
yaani Jeans, tisheti nyekundu ya Ralph Lauren na sneakers nyekundu
vinavyolingana.
Safari hiyo Trump aliifanya kama
siri kwani alionekana kutolipenda eneo hilo lililotengwa maalumu kwa ajili ya
viongozi wakubwa wa serikali ya nchi hiyo kupumzika.
Eneo hilo ambalo rais huyo
iliipeleka familiya yake lilionekana kupedwa sana kwani mkewe Melania alituama
ujumbe mfupi kwenye mtandao wa Twitter mwishoni mwa Jumamosi uliosomeka kuwa 'Barron, @POTUS na
ninafurahia Camp David nzuri! #family #sport #weekend.'
0 comments:
Post a Comment