Na Brown Mgeni
Moja ya matukio makubwa yaliyojiri mwishoni mwa wiki ni pamoja na hili la mlinzi wa Klabu ya Manchester United Phil Jones kufunga ndoa mchumba wake Kaya Hall ikiwa ni baada ya kumaliza msimu wenye mafanikio kwa kutwaa EFL Cup na Europa League.
Mlinzi huyo wa England alifunga ndoa ambayo haikuwa na mbwembwe nyingi iliyofanyika Nether Alderley, Cheshire, Ijumaa kwenye Kanisa la St. Mary’s na kuhudhuriwa na mastaa wenzake wa Manchester United wakiongozwa na Nahodha Wayne Rooney aliyeambatana na mkewe Coleen.
Wayne Rooney na mkewe Coleen (nyuma) wakiwasili kwenye harusi ya mlinzi wa United Phil Jones na Kaya Hall
Maharusi Kaya na Phil wakati wanaondoka kwenye Kanisa la St Mary’s, Nether Alderley baada ya kufunga ndoa
KABLA YA NDOA: Bibi harusi Kaya Hall akiwasili Kanisani
Bwana harusi Phil Jones akiwasili Kanisani
Coleen akionekana kumrekebisha tai mumewe Wayne wakati wanawasili Kanisani wakiwa na Chris Smalling na mchumba wake Sam Cooke
Mlinzi wa West Brom Jonny Evans akiwa na mkewe Helen McConnell ni miongoni mwa mastaa waliohudhuria kwenye ndoa ya Phil Jones
Mastaa
wengine wa soka wa United wakiwasili kwenye ndoa wakiongozwa na Luke
Shaw (Mbele kuhoto) na mlinda mlango Sam Johnstone (Katikati)
Kanisa la St Mary’s lililopo Nether Alderley ambalo Phil na Kaya walifunga ndoa
Gari lililotimiwa na maharusi
0 comments:
Post a Comment