Na Denis Massawe
Wanawake wajawazito ambao wana uzito mkubwa au unene
uliopitiliza wako hatarini kujifungua watoto wenye ulemavu hasa ulemavu
wa miguu kwa mujibu wa Watafiti wa Kisayansi wa Chuo Kikuu cha Stockholm, Sweden.
Utafiti wa Wanasayansi hao umeonesha kuwa tatizo la kuzaa watoto
walemavu hutokea iwapo mwanamke huwa mnene kabla ya kutungwa kwa mimba
ambapo kwa mujibu wa utafiti huo watoto zaidi 43,550 walizaliwa wakiwa walemavu kutokana na mama zao kuwa wanene.
Mmoja wa watafiti hao Dr. Martina Persson aliiambia Medical Journal kuwa hatari ya watoto kuzaliwa wakiwa walemavu imeongezeka kwa 4.7% huku wengi wao wakizaliwa na ulemavu wa miguu, macho, mikono na matatizo ya moyo.
Akielezea uhusiano uliopo baina ya unene na kuzaliwa kwa watoto walemavu Dr. Raul Artal
alisema wanawake wengi ambao ni wanene kupitiliza wana magonjwa kama
kisukari na shiniko la damu hivyo hupelekea watoto kutokamilika baadhi
ya viungo kutokana na presha ya mwili wa mama mjamzito.
0 comments:
Post a Comment