Na Denis Massawe
List ya mastaa wa soka barani Ulaya kuja Tanzania kutalii inazidi kuongezeka, baada ya wiki kadhaa nyuma kuja kwa David Beckham na familia yake, wiki moja baadae akatua staa wa Liverpool Mamadou Sakho, kutalii katika hifadhi ya Ngorongoro.
Baada ya mastaa hao kuja Tanzania taarifa ikufikie kuwa kuna staa wa Tottenham Hotspurs amewasili Tanzania kwa ajili ya utalii, kiungo wa timu ya taifa ya Denmark anayeichezea Totteham Hotspurs ya England Christian Dannemann Eriksen, ametua Tanzania.
Chris Eriksen amekuwa tofauti kidogo kama ilivyokuwa kwa Mamadou Sakho ambaye alikuwa haoni tatizo kupost na kuonesha kuwa yupo Tanzania, Eriksen amekuwa akipost picha bila kutaja mahali alipo ila kimuonekano yupo Ngorongoro Crater Tanzania.
0 comments:
Post a Comment