Mabingwa wa soka Tanzania bara kwa mara tatu mfululizo klabu ya Yanga wamepatwa na msiba mzito baada ya moja ya aliyekuwa mshabiki wao nguli kufariki.
Ally Yanga kama anavyofahamika amefariki hii leo mchana jijini Dodoma
ambako taarifa zinasema alikuwa kwenye shughuli za kukimbiza mwenge.
Yanga alikuwa maarufu sana katika ushangiliaji kutokana na aina yake
ya kipekee ya kujipaka mkaa usoni na kujaza nguo katika tumbo lake kama
ana kitambi.
Kutokana na msiba huo aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba bwana Haji
Manara ametuma salamu za pole kwa watani wake hao na akisema
amehuzunishwa na msiba huo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika “nimepigiwa simu kwamba
Ally Yanga amefariki huko Mpwapwa mkoani Dodoma,msiba huu ni wetu wote
na tunawapa pole watani zetu.”
Ushindi Media inatoa pole kwa Wanayanga wote pamoja na familia
ya Ally kutokana na msiba huu mzito “Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe”.
0 comments:
Post a Comment