Siku za hivi karibuni kutokana na maendeleo ya sayansi na
teknolojia ubunifu umekuwa sehemu muhimu katika maisha ya binadamu –
binadamu ambaye kila siku hufikiria kuja na kitu kipya.
Leo April 20, 2017 nimekutana na stori hii ambapo unaambiwa wabunifu wa majengo nchini Panama
wamekuja na ubunifu wa aina yake baada ya kubuni meli ambayo itatumika
kama gereza kwa ajili ya kuwafunga watu na ambayo itakuwa inatembea
baharini inayoitwa Panama Papers Jail.
Katika stori iliyochapishwa na Daily Mail April
19, 2017, wabunifu hao wamechora mchoro kwa ajili ya kutengeneza meli
kubwa ambayo itakuwa na uwezo wa kuingiza hadi wafungwa 3,300 wanawake na wanaume wakati inatembea wakisema ni mpango maalum wa kuwafunga watu wanaokwepa kulipa kodi.
Wabunifu wamesema selo za gereza hilo zitatengenezwa kwa karatasi ambazo zitatumika kama tanga kuifanya meli hiyo kutembea.
Wabunifu Axel de Stampa, Sylvain Macaux na Guillaume Devaux kutoka Ecole d’Architecture de Paris-Belleville walisema:
“Panama Papers’ Jail ni gereza lililotengenezwa kwa selo za karatasi.
Gereza linajengwa eneo la kuegeshea meli lililopo kwenye bahari ya
kimataifa likiangalia Panama City. Litakuwa na pande mbili za selo; moja
kwa wanaume na nyingine kwa wanawake.”
Meli hiyo imetengenezwa ikiwa ni sehemu ya 1week1project, tovuti ambayo hutoa wazo la ubunifu kila wiki kuhusu maisha ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment