Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, leo Ijumaa 30 Julai 2017,amezindua kituo cha kisasa cha kukusanya kodi, ushuru na tozo mbalimbali katika eneo la Simu 2000 pamoja na Kuhamsisha wafanyabiashara, bodaboda na Abiria wa Mabasi madogo .
Hii itapunguza kero kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na eneo la Simu 2000, kulipa kodi, ushuru na tozo mbalimbali ambapo awali walilazimika kwenda Kibamba zilizopo ofisi za Manispaa ya
Halmashauri ya Ubungo.
Kituo hiki kipya kinategemea kuwasaidia wakazi wa Sinza, Makurumla,
Mburahati, Mabibo, Makuburi, Ubungo na maeneo yote ya karibu.
Aidha amewataka Halmashauri ya Ubungo, kuwalinda na kuwatetea
Bodaboda dhidi ya TANROADS na JESHI LA POLISI kwa kusajili vituo vya
kupaki pikipiki na bajaji na kuwapa namba za utambuzi kwakuwa Bajeti ya
Halmashauri 2017/218, inawategemea kuwapatia Bodaboda na Bajaji kiasi
cha shillingi Billioni 4 kama chanzo cha mapato. Wakiendelea kughasiwa
Halmashauri itazikosa pesa hizo.
Amewashukuru watendaji wa Halmashauri kwa kuwajibika ipasavyo kwa
kuondoa urasimu na kutatua kero za wananchi kama ambavyo CHADEMA NA
UKAWA ilinadi majukwaani 2015.
Imetolewa na
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
HALMASHAURI YA MANISPAA UBUNGO.
0 comments:
Post a Comment