Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
imepiga marufuku matangazo ya biashara yanayowekwa mtumiaji anapopiga
simu ili kutoa fursa kwa watumiaji kupata mawasiliano bila usumbufu.
Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James
Kilaba amesema leo (Ijumaa) kuwa mamlaka hiyo imepokea malalamiko mengi
kutoka kwa watumiaji wa simu wakilalamikia matangazo hayo yanayotolewa
na kampuni za simu.
Amesema tayari TCRA imeshaziandikia
barua kampuni zote za simu kusitisha matangazo hayo na itakutana nazo
kwa majadiliano ya kina Julai 6.
Amesema mamlaka haitambui utaratibu huo
na inauchukulia kama kero kwa watumiaji wa simu ambao hutegemea kutumia
njia hiyo ya mawasiliano kurahisisha mambo.
“Tuna imani mtu anapopiga simu ana
shida ya haraka na anahitaji afanye mawasiliano, unapomuwekea matangazo
kwa dakika tatu au nne ni usumbufu,” amesema.
Katika siku za karibuni imekuwa ni
kawaida kwa mtu anayepiga simu kusikiliza wimbo au matangazo ya biashara
na baadaye kuambiwa namba anayopiga haipatikani.
0 comments:
Post a Comment