Wednesday 28 June 2017

KANISA LA MOSESI KULOLA LAVAMIWA

Kanisa la EAGT City Center la Mkuyuni Mwanza limevamiwa na kundi la watu majira ya saa 11 alfajir na kisha kubomolewa baada ya kuiba baadhi ya mali.
Mama Moses Kulola ambaye ni bibi yake Madam Flora na Mlezi wa Kanisa hilo amezungumza na moja ya chombo cha habari hapa chini  ambapo ameelezea kisa zaidi cha kuvamiwa kanisa hilo.
“Nimepigiwa simu tu kwamba wamevamia ukuta walinzi hapo mlangoni wakaanza kuwapiga na kuwaumiza. Wakaingia humu ndani na walipoingia wakaiba viti walipokimbia walinzi na mabati na maiki zote, Spika na ngoma za kwaya wamezibomoa.
“Hii ni nyumba ya Mungu. Najua heri ubomoe nyumba yangu mimi binafsi lakini nyumba ya Mungu ni jicho la Mungu. Hapa watu wanakwenda kuabudu na kuombewa, matatizo yao yanaondolewa na Mungu. Hapo atakayeshughulika na hao waliobomoa ni Mungu sio sisi.” – Mama Moses Kulola.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive