Wednesday 28 June 2017

HELKOPTA YASHAMBULIA MAHAKAMA YA JUU NCHINI VENEZUELA

Mahakama ya juu nchini Venezuela imeshambuliwa kwa maguruneti yaliyorushwa kutoka kwenye helkopta katika kile rais Nicolas Maduro amekitaja kuwa shambulizi la kigaidi.

Picha katika mitandao ya kijamii zilionyesha helikopta ya polisi ikizunguka mjini kabla ya milio ya risasi na milipuko kusikika.
Polisi ambaye alidaiwa kuiendesha ndege hiyo ya polisi iliyokuwa imeibwa alitoa taarifa ya kupinga serikali. Hadi sasa hajulikani aliko.
Kisa hiki kinajiri baada ya maandamano makubwa kupinga matatizo ya kisiasa na kiuchumi nchini humo.
Mahakama ya juu mara nyingi hukosolewa na upinzani kwa maamuzi yake ya kuchangia bwana Maduro kusalia madarakani.
Akitoa hotuba kutoka ikulu, Rais Maduro alisema kuwa helikopta ilipita juu ya mahakama ya juu na pia kwenye wizara ya sheria na ile ya mambo ya ndani.
Maafisa wanne walionukuliwa na shirika la Reuters, walisema kuwa maguruneti manne yaliangushwa kwenye mahakama na risasi 15 kufuytuliwa kuenda kwa wizara ya mambo ya ndani. 
Hakuna majeraha yaliyoripotiwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive