Beki mgumu, Vincent Bossou.
KIKOSI cha Yanga kinazidi kupukutika kwa baadhi ya nyota wa timu hiyo wanaonekana kuondoka ambapo sasa beki mgumu, Vincent Bossou raia wa Togo naye ametangaza nia ya kuondoka baada ya kugomea kusaini mkataba mpya huku uongozi ukimpa mkono wa kwaheri.
Bossou amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga ndani ya
kikosi hicho kinachonolewa na Mzambia, George Lwandamina baada ya
mkataba wake wa awali wa miaka miwili kufika ukingoni hivi karibuni.
Katibu wa Yanga, Boniface Mkwasa.
Hii inakuja siku chache baada ya beki huyo kuliambia gazeti hili kuwa yupo tayari kusaini mkataba Simba, ikiwa
viongozi wa klabu hiyo watamtafuta wakiwa na ofa nono.
viongozi wa klabu hiyo watamtafuta wakiwa na ofa nono.
Katibu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alikiambia moja ya chombo cha habari hapa nchini kuwa, wameachana na beki huyo aliyewasaidia kutwaa mataji mawili ya
ligi kuu mfululizo kutokana na yeye kushindwa kusaini mkataba mpya ambao
ungemuweka kikosini hapo licha ya kufanya jitihada za kumbakiza.
“Rasmi sasa Bossou (Vincent) hatakuwa sehemu yetu
kwenye msimu ujao wa ligi baada ya kuamua kuondoka punde tu mkataba wake
ulipofika ukingoni hivi karibuni, hivyo kumfanya awe mchezaji huru
ambaye anaweza kwenda kokote kule.
“Sisi kwa upande wetu tulipanga kuwa naye na tulifanya kila jitihada
tukiwa na lengo la kumbakiza lakini yeye ameona vyema kwenda sehemu
nyingine na hatuna njia nyingine ya kumzuia kuondoka kwa sababu
alishaamua kufanya hivyo,” alisema Mkwasa
0 comments:
Post a Comment