Kuna taarifa zilienea kwamba Jeshi la polisi Shinyanga linamshikilia kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais Magufuli kutokana na ile video fupi inayosambaa.
Ili kuufahamu ukweli, AyoTV zimemtafuta kaimu kamishna wa Polisi Shinyanga Elias Mwita
ambaye amekubali kujibu maswali na kusema Zitto hajashikiliwa na
Polisi, kilichofanya waanze kumtafuta Zitto Kabwe ni kuambiwa kwamba
anamiliki gari ambalo halina vibali halali.
SWALI: Kuna taaarifa kwamba Polisi walivamia kwenye mkutano wa hadhara aliokuwemo Zitto Kahama, kipi mlichokua mkikitafuta haswa?
JIBU LA POLISI: ‘Hiyo
ni kweli na ni baada ya Polisi kupata taarifa za kiintelijensia kwamba
Zitto anamiliki gari ambalo halina vibali halali lakini kabla
hatujakutana nae Zitto Kabwe akawa ametoweka kwenye eneo hilo na
kulitelekeza lile gari, baadae alipatikana Dereva wake tukaomba hizo
documents na hazikuwepo’
SOURCE: AYO TV
0 comments:
Post a Comment