Ripoti mpya kutoka The Independent na ParsToday zinasema kuwa Rais Donald Trump
wa Marekani amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na
wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa ambapo uamuzi huo umefanyika
katika siku yake ya kwanza kazini.
Trump ambaye aliapishwa Ijumaa January 20, 2017 kuwa Rais wa 45 wa
Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtangulizi wake, Barack Obama kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muda wa kujitayarisha kuondoka kama ilivyo kawaida.
Inaelezwa
kuwa zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi mbalimbali duniani
walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana ikiwa ni
mara baada ya Trump kuapishwa.
Hatua hiyo
ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na washirika muhimu kama vile
Ujerumani, Uingereza na Canada ambapo ripoti zinasema nchi hizo zinaweza
kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya Trump kuteua
mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Congress kabla ya
kuanza kazi zao.
Donald
Trump anakosolewa kwa kuacha nafasi nyingi wazi na hivyo kuvuruga
shughuli za kawaida za serikali ya Marekani na hii haya yanajiri huku
maandamano yakiripotiwa kuendelea sehemu mbalimbali kupinga utawala wa
kiongozi huyo.
Nchini
Marekani katika siku ya pili ya utawala wa Trump kumeripotiwa maandamano
ya watu milioni tatu na imeripotiwa kumefanyika maandamano 637 katika
maeneo mbalimbali ya Ulaya, Asia na Afrika kumpinga rais mpya wa
Marekani.
0 comments:
Post a Comment