Tuesday, 24 January 2017

RAIS MAGHUFULI KUZINDUA MAGARI YAENDAYO KASI SIKU YA KESHO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. John Pombe anatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa huduma ya mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam siku ya kesho.

Uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika kwenye stendi kuu ya mabasi hiyo ya Gerezani jijini Dar es Salaam, utaanza majira ya asubuhi.

Kwa mujibu wa matangazo yanayotolewa na kampuni inayosimamia mradi huo ya UDART, rais Magufuli anatarajia anatarajiwa kuzungumza na wananchi watakaojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Mabasi ya mwendo wa haraka maarufu kama ‘Mwendo Kasi’ yalianza kazi mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka jana baada ya kukamilika kwa zoezi la majaribio ya utoaji huduma pamoja na kupangiwa njia za kusafirisha abiria.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive