
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamduni na Michezo Nape Nnauye
Kwenye vitu vilivyoleta mjadala mkubwa kwenye mitandao ya
kijamii Wikiend iliyopita ni pamoja na suala la Waziri wa
Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Nape Nnauye kumkabidhi Bendera ya
Taifa, Diamond Platnumz ambaye alikua anaelekea Gabon kwa ajili ya kutumbuiza kwenye ufunguzi wa michuano ya kombe la Afrika (Afcon 2017).

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete.
Baada ya Diamond kufika Gabon ilipigwa picha ya pamoja na wasanii
mbalimbali walioenda kutumbuiza wakiwa na bendera za nchi zao,baada ya
picha hiyo Waziri wa Habari Nape kupitia twitter aliandika >>’Ulizeni tena kwanini nilimkabidhi bendera Diamond‘ akamaliza na ki-alama cha kushangaa.

Mara baada ya tukio la kukabidhiwa bendera ya taifa Diamond Platnumz
kabla ya kuelekea Gabon,Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete aliandika
kuhusu kushangazwa na hali hiyo na aliandika >>’TFF
nadhani mnajua kuwa Mungu wa Watanzania anawaona.Tumefika hapa baada ya
mpira kutushinda kabisa.Sasa tunatoa Bendera kwa wanaokwenda
kuburudisha na sio wanamichezo tena……..Ngashindwa mie’.


0 comments:
Post a Comment