JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limepiga marufuku uuzwaji
holela wa silaha za jadi kama vile, manati, pinde na mikuki huku
likisema tayari limemkamata mtuhumiwa mmoja katika maeneo ya mataa ya
Tazara, Mgoli Sakalani(39) akifanya biashara hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es
Salaam, Simon Sirro, alisema kuwa tabia hiyo imejengeka kwa
wafanyabiashara wadogowadogo ambao wamekuwa wakiuza silaha mbalimbali
zikiwemo mapanga, manati,visu na upinde pembezoni mwa barabara.
Kamanda Siro amewataka wafanyabiashara hao kuacha mara moja biashara hiyo
ambayo imeshamiri sana katika Barabara ya Nyerere kwenye Mataa ya
Tazara,Mataa ya Chang’ombe na Mataa ya Gerezani.
Alifafanua kuwa miongoni mwa wauzaji wa bidha hizo wengi wao siyo
waaminifu kwani hutumia fursa hiyo kuwatishia watu wakiwa kwenye magari
binafsi,magari ya umma na kisha kuwaibia mali mbalimbali kama vile simu
za mkononi,saa,mikoba na laptop.
Kamanda huyo ametoa rai kwa wafanyabiashara hao kuifanya biashara hiyo
sehemu maalumu kama madukani wakiwa na leseni ya biashara,vinginevyo
atakayepatikana akifanya biashara hiyo kiholela atachukuliwa hatua za
kisheria.
Katika hatua nyingine, Kamanda Sirro amesema kesho Jumamosi ni siku ya
Polisi ijulikanayo kama ‘Polisi Day’ ambapo wataadhimisha siku ya
familia katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar, huku mgeni rasmi
akitarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.
Amesema baada ya hafla hiyo fupi, waziri huyo akiambatana na baadhi ya
viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, wataelekea katika mikoa
ya Kipolisi ya Kindondoni,Temeke na Ilala ambapo watatembelea
Hospitaliza Mwananyamala, Amana na Temeke kushiriki kufanya usafi wa
mazingira maeneo hayo.
Maandhimisho hayo ya siku ya familia pia yataambatana na burudani ya
ngoma za asili,kuvuta kamba, kukimbiza kuku na muziki kutoka bendi ya
polisi.
0 comments:
Post a Comment