Rais John Magufuli amesema vyombo vya habari vinavyopotosha ukweli na
kuleta uchochezi siku zake zinahesabiwa kwani Serikali yake anayoiongoza
haiwezi kukubali kuvurugwa kwa amani ya nchi.
Amesema mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 chanzo
chake ni vyombo vya habari, hivyo hawezi kukubali hali hiyo itokee
nchini.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda cha Jambo Food Plant mjini
Shinyanga na matangazo yake kurushwa mubashara na Star Tv, Rais Magufuli
amesema magazeti yote isipokuwa mawili, vituo vyote vya televisheni na
redio nchini vinafanya kazi nzuri ya kuelimisha wananchi.
Rais Magufuli amesema Serikali yake haikatai kukosolewa na kwamba,
magazeti mengine yanakosoa na kusaidia kutatua matatizo ya jamii, lakini
hayo mawili (bila kuyataja) yamekuwa ni kupindisha kila kitu.
“Hayo magazeti kila ukisema hivi yanapindisha, siyataji kwa sababu yanajifahamu lakini yajue kwamba siku zake zinahesabika. Serikali ninayoiongoza haiwezi kukubali amani kuvurugwa,” amesema.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment