WAKATI wakielekea kumaliza mwaka 2016 bila ndoa, wasanii hawa
wamekuwa mvuto mkubwa kwa mashabiki wao huku wengi wao wakiwatarajia
ndoa kwa mwaka ujao wa 2017.
Diamond na Zari
Mapenzi ya msanii Nassibu Abdul (Diamond) na mwanadada kutoka Uganda,
Zarinah Hassan (The Boss lady), yameboreshwa zaidi baada ya kuishi
zaidi ya miaka mitatu na kupata watoto wawili wa kike na wa kiume.
Licha ya kutokufanikiwa kufunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake Miss
Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, mashabiki wake wengi wanamtarajia
mwaka 2017 atimize ndoto hiyo kwa mpenzi wake wa sasa Zari ambaye ni
mwanamuziki na mfanyabiashara.
Ali Kiba na Jokate
Licha ya wapenzi Ali Kiba na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kupitia katika
uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali wa ndani na nje ya nchi,
wawili hao wameonekana kuwavutia mashabiki wao hasa wanapokuwa pamoja
mijumuiko mbalimbali ikiwamo kwenye sherehe, mpira na mingine mingi.
Ali Kiba anayejishughulisha na sanaa ya uimbaji kwa sasa anatamba na
wimbo wake wa ‘Aje’, huku Kidoti akijishughulisha na masuala ya urembo
ikiwamo biashara ya nywele, ndala, nguo na muziki wapo katika mastaa
wanaodhaniwa kufunga ndoa mwakani sasa ni je, nao watafunga ndoa mwaka
2017 kama wanavyodhaniwa na wengi?
Nahreel na Aika
Hawa ni wapenzi wanamuziki wa muda mrefu tangu walipokutana nchini
India walipokuwa masomoni, uhusiano wao umeongeza uimara katika kundi
lao la Navy Kenzo. Nahreel jina lake kamili ni Emmanuel Mkono na Aika
Marealle.
Zaidi ya miaka nane katika uhusiano wa kimapenzi ndio unaowavutia mashabiki wao wakitamani wapenzi hawa waoane 2017.
Jux na Vanessa
Wapenzi hawa walianza muda mrefu tangu Jux alipoachana na Jack ambaye
sasa anatumikia kifungo huko China. Wawili hawa wanatamba na wimbo wao
wa Juu. Ukaribu wao na picha za kimapenzi kila wanapokuwa mapumzikoni
huku kila mmoja akiwa wazi kumuelezea mwenzake inaonekana kuwa chachu ya
wawili hao kuwa pamoja katika ndoa, Je, wawili hawa watafunha ndoa
mwakani huku kila mmoja akionekana kuzidi kutotaka kubadili dini
kumfuata mwenzake?
Lady Jaydee na Spicy
Baada ya mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kuachana na
aliyekuwa mume wake mtangazaji, Guardina G. Habashi maarufu Captain,
sasa ameangukia katika penzi la prodyuza na mwanamuziki raia wa Nigeria,
Spicy.
Licha ya mapenzi, wawili hao kwa sasa wanatamba na wimbo wa ‘Together
Remix’, ukaribu wao na namna wanavyozungumzwa kwenye mitandao ya
kijamii pamoja na watu wao wa karibu, je, nao watafunga ndoa mwaka 2017?
Lulu na Majizo
Mbwembwe na vituko vingi vya mwigizaji, Elizabeth Michael ‘Lulu’,
vinaonekana kufikia mwisho baada ya kudondokea kwenye mapenzi na mwasisi
wa kituo cha redio Efm mwenye umaarufu wa jina la Dj Majizo.
Majizo
anaelezwa kummiliki vyema mrembo huyo kiasi kwamba tabia na matukio ya
utata yaliyokuwa yakimwandama mrembo huyo hayaonekani kwa sasa. Je, nao
watafunga ndoa mwaka 2017 kama wanavyodhaniwa na wengi?
Moses Iyobo na Aunt Ezekiel
Mapenzi ya mcheza dansi wa Nasibu Abdul, ‘Diamond Platinumz’, Moses
Iyobo na mwigizaji Aunt Ezekiel yanazidi kusonga mbele huku mtoto wao
akiongeza upendo kati ya wawili hao kiasi kwamba muda wote wanatamani
kuwa karibu naye.
Anty Ezekiel kabla ya kudondokea kwa Mose aliolewa na mfanyabiashara
wa magari anayefahamika kwa jina la Papaa Sunday Demonte, ambaye kwa
sasa anatumikia kifungo huko Dubai. Je, nao watafunga ndoa mwaka 2017
kama wanavyodhaniwa ama la?
Shilole na Adam Suleiman
Mwigizaji, mwanamuziki na mama ntilie, Zuwena Mohamed (Shilole) baada
ya kumwagana na Nuh Mziwanda kwa sasa amedondokea kwa mfanyabiashara wa
nguo, Adam Suleiman ambaye kiumri anaonekana kuwa mkubwa zaidi ya
Shilole ambaye awali alikuwa akisemwa vibaya kwa kuwa na uhusiano na
wanaume wenye umri mdogo.
Umri na namna ambavyo mfanyabiashara huyo kutokuwa maarufu kunaelezwa
kuwa ni sababu kubwa ya wawili hao kufika mbali katika uhusiano wao
kiasi kwamba huenda wakaoana mwaka 2017.
Harmonize na Wolper
Msanii wa Bongo Fleva kutoka Kundi la Wasafi, Rajabu Ibrahim (Harmonize) na Jackline Wolper,
licha ya maneno ya kukatisha tamaa wapenzi hawa wamekuwa wakiendelea na
maisha yao bila kujali maneno ya watu, je, nao watafunga ndoa mwaka
2017 kama wanavyodhaniwa?
Giggy Money na Moj
Wapenzi hawa Giggy Money na Moj walianza uhusiano wa kimapenzi muda
mrefu wakati Moja akimtumia Giggy kumpata rafiki yake na ikawa hivyo,
lakini baada ya kukutana pamoja katika kipindi cha Usiku redio ya Choice
FM wakaanza kupendana zaidi hadi sasa ni wapenzi.
Giggy kwa sasa amepunguza upigaji wa picha za hovyo kutokana na kazi
anayoifanya na aina ya mwanaume aliyenaye, huku kazi yake ikimpa nafasi
ya kukutana na watu wenye nyadhifa mbalimbali. Kutokana na hayo wapenzi
hawa watafunga ndoa mwaka 2017?
Young Dee na Mamisa
Licha ya rapa David Genzi kurudi kwa mpenzi wake wa muda mrefu mwenye
umaarufu kwa jina la Tunda na kutoka na wimbo mpya unaoeleza kutamani
kwake kumuoa, lakini inaonyesha kama imeingia dosari kwa kuwa mashabiki
wengi wanatamani rapa huyo amuoe mwanamke mwingine anayefahamika kwa
jina la Mamisa ambaye amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuweka wazi
kwamba amemzalia mtoto rapa huyo ambaye awali hakuonyesha kujali, lakini
baada ya kuweka wazi alijitokeza na kutoa matunzo ya mtoto wake. Je,
nao watafunga ndoa mwaka 2017 kama wanavyodhaniwa na wengi?
Witness na Ochu
Kutokana na ukaribu na kuelewana katika muziki wanaofanya na mambo
mengine, rapa wa kike, Witness maarufu ‘Kibonge mwepesi’ na mpenzi wake
wa muda mrefu mwanamuziki, Ochu Sheggy, nao wanatamaniwa na mashabiki
wao wafunge ndoa, je, nao watafunga ndoa mwaka 2017 kama wanavyodhaniwa
na wengi?
0 comments:
Post a Comment