Mkuu wa wilaya ya Kigamboni
Hashim Mgandilwa ameanza ziara ya kutembelea Kata za Wilaya ya
Kigamboni, ambapo ameanzia Kata ya Kimbiji na kuzindua vyumba vitatu vya
madarasa katika shule ya msingi Bohari.
Mapema akizindua vyumba vya
madarasa DC Mgandilwa aliingia madarasani na kukuta mahudhurio ya
wanafunzi hayaridhishi huku kukiwa hamna taarifa yoyote kwa Mwalimu Mkuu
juu ya ruhusa au wanafunzi wagonjwa.
Kufuatia utoro huo wa
wanafunzi DC Mgandilwa amewaweka ndani wazazi (2) wa wanafunzi hao na
kuagiza wazazi wengine wa wanafunzi watoro ambao hawakuwepo mkutanoni
kutafutwa na kukamatwa kwani utoro huo unasababishwa na wazazi.
Ziara aliyoianza leo DC
Mgandilwa inalenga kushirikiana na wananchi katika shughuli za
kimaendeleo, kusikiliza na kutatua kero zao moja kwa moja katika maeneo
wanayoishi.
0 comments:
Post a Comment