Home »
KITAIFA
» TAARIFA KUSUHU KUPUNGUA KWA VIFO WAZAZI NA WATOTO
Tanzania imepiga hatua kubwa
katika kuboresha huduma za uzazi wa mpango nchini tofauti na kipindi cha
nyuma ili kuweza kuondoa idadi ya ongezeko kubwa la watu na kupunguza
vifo kwa wajawazito na watoto kama Sera ya Afya ya mwaka 2007
inavyosema.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati
akifungua mkutano wa bodi kwa nchi zilizoamua kuongeza idadi ya watu
wanaofahamu uzazi wa mpango kundi linalojulikana kama “FP 2020 Reference
Group”.
“Tanzania
imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma za uzazi wa mpango nchini
tofauti na kipindi cha nyuma ili kuweza kuondoa idadi ya ongezeko kubwa
la watu na kupunguza vifo kwa wajawazito na watoto kama sera ya Afya ya
mwaka 2007 inavyosema” amesema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema
mkutano huu unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na hususani
katika ardhi ya Tanzania hii ni kutokana na mafanikio makubwa
yaliyofikiwa katika eneo hili la uzazi wa mpango . Mkutano huo wa siku
tano ulioanza Oktoba 31 hadi Novemba 4 mwaka huu unahudhuriwa na
wajumbe na wadau kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwa na lengo la
kujadili fursa mbalimbali na changamoto zilizopo katika eneo la afya ya
uzazi wa mpango duniani.
Waziri Ummy amesema mafanikio
hayo ni pamoja na ongezeko la bajeti katika eneo la uzazi wa mpango na
kupunguza hali ya utegemezi kwa kiasi kikubwa kutoka kwa wahisani,
kuimarisha mìfumo ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba za uzazi wa mpango
hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya uzazi
wa mpango Dk. Babatunde amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya
Tanzania katika kuhakikisha huduma hii inaimarika.
0 comments:
Post a Comment