Home »
KITAIFA
» AGIZO LA JPM LAWATOA JASHO WAHUDUMU WA VYOO
AGIZO
la Rais John Magufuli la kuwataka wananchi kudai au kutoa risiti pindi
wanapouza au kununua bidhaa, limewatoa jasho wafanyabiashara wanaotoa
huduma za choo katika jiji la Mwanza.
Katika kutekeleza agizo hilo,
wafanyabiashara hao wamesema wananchi wanaopata huduma katika baadhi ya
vyoo vya kulipia, wamekuwa wakitaka wapewe risiti za kielektroniki (EFD)
badala ya zile za karatasi.
Hatua hiyo imetokana na baadhi ya
wazabuni wanaoendesha huduma za vyoo kutumia risiti za Halmashauri ya
Jiji la Mwanza kwa kuwa vyoo hivyo viko chini ya halmashauri hiyo.
Msimamizi wa choo kilichoko maeneo ya
Makoroboi, jijini hapa, Masoud Masib, alisema wao wanatumia risiti
kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa sababu vyoo hivyo viko chini ya
halmashauri.
0 comments:
Post a Comment