Tuesday, 12 September 2017

ZITTO,KUBENEA WASAKWA

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuagiza kutafutwa kwa namna yoyote Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea apelekwe kesho kwenye Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ili ahojiwe kuhusu kauli aliyoitoa ya kumtuhumu Spika kuwa amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),  Tundu Lissu.
Pia  Spika Ndugai ameagiza Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka kwa tuhuma mbili tofauti                      

Zitto anatuhumiwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili fulani, wakati Kubenea ni kwa kumtuhumu Spika kusema uongo wa idadi ya risasi alizopigwa Lissu.

Spika Ndugai ametoa maagizo hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive