Tuesday, 19 September 2017

TRUMP AWAPA UJUMBE HUU KOREA KASKAZINI

Rais wa Marekani Donald Trump ameonya vitisho kutoka kwa mataifa Korea kaskazini na Iran katika hotuba yake katika umoja wa mataifa.
Katika hotuba yake ya kwanza katika mkutano wa umoja huo mjini New York, ameonya kuwa Marekani itaangamiza Korea kaskazini iwapo italazimika kujitetea ama kuwalinda washirika wake.

Alimkejeli kiongozi wa Korea kaskazinmi Kim Jong un akisema: Yuko katika harakati za ''kujitoa muhanga''.

Korea kaskazini imefanya makombora yake kinyuklia majaribio na kukiuka maamuzi ya Umoja wa mataifa.

Iran, bwana Trump alisema ni nchi ya kifisadi na inayoongozwa kidikteta kwa lengo la kutaka kuyumbisha eneo la mashariki ya kati.

Ameitaka serikali mjini Tehran kukoma kuwasaidia ugaidi mbali na kuukosoa utawala wa rais Obama kuhusu makubaliano ya mpango wa amani wa nyuklia wa taifa hilo ambao ameutaja kuwa aibu.

Amesema kuwa marekani haitanyamaza ama kuingia mikataba inayopendelea upande mmoja.
Amesema kuwa mataifa mengine yanaelekea motoni lakini akasema kuwa UN utayasaidia.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive