IWAPO amani ya mawazo au
akili inamaanisha kutembea kwa utulivu nyumbani ukipita kwenye miti na
maua, kuwa na fedha za kutosha benki, kuwa na kazi ya uhakika, mahali
bora zaidi kwa kupata amani hiyo ni katika miji ya nchini Ujerumani.
Utafiti
mpya umeonyesha miji yenye utulivu zaidi ya mwaka 2017 kwa kutia
maanani usafiri wa barabarani, usafiri wa umma, maeneo ya kupumzikia na
bustani, hali za kifedha za watu wake ikiwa pamoja na viwango vya
madeni, afya ya kimwili na kiakili na saa ambazo miji husika hupata
mwanga wa jua kwa mwaka.
Katika
miji 150 iliyohusika, miji minne ya kwanza miongoni mwa kumi isiyokuwa
na matatizo ni ile ya Ujerumani. Mji wa kusini mwa nchi hiyo wa
Stuttgart ndiyo unaongoza orodha hiyo, Hanover ukishika nafasi ya tatu,
Munich wa tano na Hamburg ukishika nafasi ya tisa na Graz wa Austria.
Nchi ndogo yenye utajiri
mkubwa ya Luxembour inayokaliwa na watu wasiozidi 600,000, ndiyo
inashika nafasi ya pili duniani. Mji wa Bern nchini Switzerland unashika
nafasi ya nne, Bordeaux (Ufaransa) wa sita, Edinburgh, Uingereza wa
saba.
Sydney, Australia (wa
nane) ukiwa mji pekee usiokuwa wa Ulaya kuingia katika kumi bora wakati
ambapo Seattle ndilo jiji lenye mazingira bora yasiyo ya joto nchini
Marekani.
Utafiti huo uliofanywa na
shirika moja la Uingereza liitwalo Zipjet, ulijumuisha maeneo 500 yenye
kuhusisha aina 17 za mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na
miundombinu, viwango vya uchafuzi wa mazingira, fedha na hali za raia
wake.
Kwa upande wa miji yenye
matatizo na wasiwasi, Baghdad wa nchini Iraq unashika nafasi ya kwanza
ukifuatiwa na Kabul (Afghanistan) ambapo Lagos nchini Nigeria barani
Afrika, unashika nafasi ya tatu.
Mji miwili ya Afrika,
Dakar (Senegal) na Cairo (Misri) inashika nafasi ya nne na tano katika
orodha hiyo, ikifuatiwa na Tehran (Iran) inayoshika nafasi ya sita,
Dhaka ya Bangladesh (nafasi ya saba) na Karachi wa Pakistan unaoshika
nafasi ya nane. Miji ya New Delhi wa India na Manila (Philippines)
inashika nafasi ya tisa na kumi katika orodha hiyo.
Katika utafiti huo pia
palibainika kwamba Luxembourg una idadi ndogo zaidi ya watu ukifuatiwa a
Kuwait City, wakati ambapo Sydney na Melbourne inayoshika nafasi ya
sita na saba, maeneo yake hayana msongamano wa watu.
Kwa upande huohuo wa
mazingira barani Afrika, Abidjan nchini Ivory Coast ndiyo una kiwango
cha chini zaidi cha uchafuzi wa mazingira kwa upande wa sauti ambapo
Antananarivo (Madagascar) una kiwango cha chini zaidi katika uchafuzi wa
mazingira wa mianga wakati wa usiku, jambo linalofanya kushindikana
kuonekana kwa nyota na sayari mbalimbali angani nyakati za usiku.
0 comments:
Post a Comment